You need to be logged in to post in the forums. If you do not have an account, please sign up first.
Vijana wa Kitanzania
Nadhani sisi ndio tunaotegemewa kama taifa la leo ambalo linapaswa kuwawekea muongozo mzuri wadogo zetu ambao ndio taifa la kesho.Utakuta kuna vijana pamoja na kusema ni wa kiume huwa wanafanya mambo ya wanawake kama kutoboa maskio,kusuka nywele na mengineyo, hiyo itamfunza nini mdogo wako?
Kuna wengine hupenda kuvalia suluari chini ya kiuno mpaka nguo zao za ndani kuonekana, jamani hiyo ni aibu ambayo sitopenda tuiendekeze kwani tupo kwa ajiri ya kuelimishana sio kuwaaribu wadogo zetu kihisia.
Hivyo nawaomba vijana wenzangu tujirekebishe ili tuweze kujenga taifa lenye kuendana na maadili ya Kitanzania.
By Japhet K..
thats true Man Mswahli,youths hv gone