By John leonardjleonny. Monday, May 21, 2012 6:22:37 AM
ee mwenyezi mungu,muumba nchi na mbingu.niondolee ukungu wa haya maisha magumu.niondolee uthubutu,wakuweza kubwia sumu.ni kama upatu,uliogandana kutu au kisu kisichobutu,koromeoni mwa mtu au mtutu uliodiriki kudhubutu kuibeba risasi kuundoa uhai wa mtu.na hustle kila siku,naishia kuambulia buku,wekundu hunitosha kwa siku,niondokane na life la kunguru.ndio bongo huku,ujiruzuku kwa kuishika sururu.wametususa zetu ndugu,tulio wapeleka ikulu.maisha yao ya juu,daily wakila kuku.wametusahau wa huku,na maisha yetu ya huku.wameyafanya magumu na mbaya ya kudumu.ee nyoka kifutu,twajiponya na zako sumu.nakupiga virungu,maneno yangu ndio sumu.ubadhirifu wako kila siku,kutupa maisha magumu.














Ahmadi Mmambeammambe # Wednesday, May 23, 2012 4:37:51 PM
stevElevensteveleven # Wednesday, May 30, 2012 9:54:25 PM
John leonardjleonny # Friday, July 13, 2012 11:42:53 AM
John leonardjleonny # Friday, July 13, 2012 11:44:31 AM